Victoria government logo

Kwani watoto wanapaswa kusonga zaidi (Why kids need to get their move on) - Kiswahili (Swahilli)

Ili kukuza tabia nzuri, watoto na vijana wanapaswa kusonga zaidi. Soma kuhusu kiasi cha shughuli ambayo watoto na vijana wanapaswa kufanya kila siku, na faida zake.

Kwani watoto wanapaswa kusonga zaidi

Inapendekezwa kamba watoto wa umri wa miaka 5 hadi 12 na vijana wa miaka 13 hadi 17 wafanye mazoezi ya viungo kwa dakika 60 kila siku. Ili kusaidia kurahisisha hili, tunapendekeza kuyagawanya katika dakika 15, mara 4 kwa siku.

Mazoezi ya viungo ni kitu chochote kinachosonga mwili wako, hukufanya upumue haraka na huongeza mapigo ya moyo wako. Mazozi ya viungo huwafanya watoto wawe na furaha na afya njema, na huwasaidia kukuza tabia nzuri katika maisha yote.

Kusonga kila siku kuna faida nyingi, ikiwemo:

  • kuboresha afya kwa ujumla
  • nguvu zaidi
  • hatari ndogo ya afya duni, magonjwa na kuongezeka kwa uzito usiofaa
  • viwango vizuri vya shinikizo la damu, lehemu na viwango vya sukari kwenye damu
  • kufurahi pamoja na marafiki na familia
  • tabia chache isiyo ya kijamii
  • ushirikiano zaidi na ujuzi wa kazi ya timu
  • kujithamini na kujiamini vizuri sana
  • wasiwasi na mfadhaiko mdogo zaidi
  • umakini mzuri zaidi
  • ukuaji na maendeleo mazuri
  • misuli na mifupa yenye nguvu
  • utimamu wa mwili, uratibu na mwendo thabiti

dakika 15, mara 4 kwa siku

Tunapendekeza mazoezi ya viungo yafanyike mara nne kwa siku kwa dakika 15.

Mazoezi haya yanaweza kujumuisha mambo kama:

  • kutembea au kuendesha baisikeli shuleni au kuzunguka maeneo yalio karibu yako
  • kumtembeza mbwa
  • kwenda kwenye bustani na marafiki
  • soka
  • mchezo wa kuteleza kwenye ubao
  • kucheza katika uwanja wa nyuma
  • tenisi
  • kuogelea
  • kucheza ngoma
  • kukimbia au kukimbia polepole
  • mpira wa kikapu
  • kupanda
  • yoga
  • kuinua vitu vizito
  • netiboli

Reviewed 07 December 2022

Education

Was this page helpful?