Chekechea ya Bure inapatikana katika programu za Chekechea za Umri wa Miaka Mitatu na Minne au za Maandalizi ya Chekechea kwenye huduma za kushiriki kote Victoria. Hii ni pamoja na huduma za utunzaji wa siku nzima na huduma za chekechea za pekee (ambazo pia huitwa huduma za muda).
Akiba kwa familia
Familia zenye watoto walioandikishwa katika chekechea za muda cha kushiriki zinapata programu ya bure.
Familia zenye watoto walioandikishwa katika huduma ya matunzo ya siku ndefu inayoshiriki zinapata malipo ya ada ya mwaka.
Ustahiki wa Chekechea ya Bure
Chekechea ya Bure ni kwa kila mtu.
Familia hazihitaji kuwa na Kadi ya Huduma ya Afya (Health Care Card) au Kadi ya Pensheni, uraia wa Australia, au uthibitisho wa anwani ili kustahili kupata huduma. Pia huhitaji kustahili Ruzuku ya Huduma ya Utunzaji wa Watoto ya Serikali ya Australia (CCS) ili kupokea Chekechea ya Bure.
Unaweza tu kupokea Chekechea ya Bure katika huduma moja ya Chekechea kwa wakati mmoja. Huduma yako ya chekechea itakuuliza utie saini kwenye barua, ikitaja huduma ambayo utapokea Chekechea kwa Bure. Ikiwa mtoto wako anahudhuria zaidi ya huduma moja ya chekechea, unapaswa kujulisha kila huduma unapotaka kupata Chekechea ya Bure.
Jinsi ya kupata ufadhili wa Chekechea ya Bure
Huduma za Chekechea zinazotoa Huduma za Chekechea ya Bure hupokea ufadhili moja kwa moja kutoka kwa Serikali ya Victoria. Hii ina maana kwamba familia si lazima zidai kurudishiwa akiba, badala yake ada zako zitapunguzwa. Katika chekechea ya muda programu yako ni bure.
Familia zinazotumia programu za chekechea za kulelea watoto kwa kutwa nzima zitaweza kuona akiba kutokana na Chekechea ya Bure kila kipindi cha madai chenye ‘Punguzo la Chekechea ya Bure la Serikali ya Victoria’ ikiwa imeandikwa kwa uwazi kwenye ankara (karatasi ya madai).
Jinsi punguzo la malipo ya ada linalotumika kwa ada zako za nje ya matumizi ya kawaida
Punguzo la malipo ya Chekechea ya Bure yatatumika kwa ada zako mara kwa mara mwaka mzima (k.m. kila wiki au wiki mbili). Unapaswa kuweza kuona kiasi kilichoelezwa kwa uwazi kwenye ankara yako kama ‘Punguzo la Chekechea ya Bure la Serikali ya Victoria’.
Kwa maelezo kuhusu jinsi punguzo la malipo yatatumika kwa ada zako na jinsi hii inavyoonyeshwa kwenye ankara yako, tafadhali zungumza moja kwa moja na huduma yako ya chekechea. Ikiwa mtoto wako anapata zaidi ya saa 15 kwa wiki, saa hizi za ziada hazijashughulikiwa na punguzo la malipo.
Kama unastahili kwa Ruzuku ya Utunzaji wa Watoto ya Jumuiya ya Madola hiyo itatumika kwanza. Hiyo ina maana kwamba utahitaji tu kulipa kiasi kilichosalia baada ya CCS na baada ya punguzo la Chekechea ya Bure.
Mfano:
- Mtoto mwenye umri wa miaka 4 huenda kwenye huduma ya siku ndefu yenye programu ya chekechea kwa siku 3 kwa wiki.
- Huduma hutoza $360 kwa siku 3 ya wiki (ikiwa ni pamoja na saa za chekechea na saa ziada za matunzo).
- Familia inapata CCS ya $252 kwa wiki.
- Katika 2025, huduma huomba malipo ya $2,101 ya Chekechea ya Bure kwa wiki kwa wiki 40 ($52.53 kwa wiki).
- Familia hulipa $55.478 kwa wiki baada ya malipo ya CCS na Chekechea ya Bure.
Tafadhali kumbuka. Hii ni mfano tu na gharama zitatofautiana kutegemea hali za mtu na kiasi cha malipo ya kila mwaka ya Chekechea ya Bure.
Updated