Three-Year-Old Kindergarten brochure - Swahili

Serikali ya Victoria inawekeza karibu dola bilioni $5 kwa muongo mmoja kuanzisha Chekechea ya Miaka Mitatu inayofadhiliwa kwa wote - na sasa inapatikana kote jimboni.

Serikali ya Victoria inawekeza karibu dola bilioni $5 kwa muongo mmoja kuanzisha Chekechea ya Miaka Mitatu inayofadhiliwa kwa wote - na sasa inapatikana kote jimboni.

Hii inamaanisha kuongezeka kwa mwaka mwingine wa kujifunza, kukua, kucheza na kupata marafiki kwa watoto wa Victoria.

Kushiriki katika mpango bora wa chekechea kutoka umri wa miaka mitatu huongeza ujifunzaji wa watoto, maendeleo, afya na matokeo ya ustawi.

Watoto wadogo hujifunza juu ya dunia inayowazunguka kupitia kucheza

Kujifunza kwa njia ya kucheza ni jinsi ambavyo watoto wadogo wanavyajifunza vizuri. Inawapa watoto nafasi ya kutumia mawazo yao, kujenga ustadi wao wa lugha na kujifunza juu ya nambari na mifumo. Wanajifunza pia jinsi ya kuelewana na wengine, kushiriki, kusikiliza na kudhibiti hisia zao.

Watoto wote katika Victoria wanaweza kupata miaka miwili inayofadhiliwa ya Chekechea

Watoto kote jimboni watafaidika kuanzia 2022 na kupata angalau masaa matano ya mpango wa chekechea uliofadhiliwa kila wiki. Masaa yataongezeka hadi masaa 15 kwa wiki kufikia 2029.

Bila kujali mahali ambapo mtoto anaenda kwenye checkechea, walimu na waalimu waliofunzwa wataongeza mpango

Watoto wanaweza kuhudhuria programu ya chekechea katika huduma ya siku ndefu (huduma ya watoto) au kwenye chekechea ya kawaida.

Watoto wadogo wanajifunza kuhusu dunia kupitia kucheza

Wanajifunza jinsi ya kuelewana na wengine, kushiriki, kusikiliza na kudhibiti hisia zao

Katika programu ya checkechea, watoto wanatumia michezo kujenga ustadi wao wa lugha na kujifunza juu ya nambari na mifumo

Walimu na waelemishaji husaidia watoto kuwa mdadisi, mbunifu na ujasiri juu ya kujifunza

Updated