Victoria government logo

Usaidizi wa Kifedha na Chekechea ya Kuanza Mapema (Financial Assistance and Early Start Kindergarten) - Kiswahili (Swahili)

Serikali inatoa ufadhili kwa watoto wote kuhudhuria miaka miwili ya programu ya chekechekea. Huduma nyingi hutoza ada pamoja na ufadhili wa serikali. Familia yako inaweza kupata usaidizi wa gharama hii. Ikiwa unatoka kwenye asili ya ukimbizi au mtafuta hifadhi, programu inayoitwa Chekechea ya Mwanzo ya Mapema (ESK) inapatikana pia. ESK inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa unapata kiwango cha juu zaidi kinachowezekana cha saa za mpango wa chekechea bila malipo kila wiki kwa ajili ya mtoto wako.

Mnamo 2023, programu za Chekechea ya Mtoto wa Miaka Mitatu ni za kati ya saa 5 na 15 kila wiki na programu za Mtoto wa Miaka minne ni za saa 15. Kujiandikisha kupitia ESK kunakuhakikishia saa 15 kamili kila wiki katika programu za Chekechea ya Watoto wa Miaka Mitatu na Miaka minne. Inapatikana kwa watoto ambao:

  • wanatoka katika mazingira ya mkimbizi au mtafuta hifadhi
  • wanaojitambua kama Waaboriginal na/au Torres Strait Islander
  • ambaye familia yake imewahi kuwa na mwingiliano na ulinzi wa mtoto(child protection)

Haijalishi ni wapi wanaishi Victoria watoto hawa wanaweza kupata saa 15 bila malipo au chekechea ya bei ya chini kwa wiki wakati wa kipindi cha kuanzisha hii programu. Ufikiaji wao wa sasa na saa wanazopokea hazitabadilika.

Jinsi ya kuomba:

ESK inapatikana katika programu zote za chekechea zinazotolewa na mwalimu aliyehitimu. Unaweza kumwandikisha mtoto wako kwa kuwasiliana na chekechea iliyo karibu nawe na kuomba kupata ruzuku ya Chekechea ya Awali ya Mwanzo. Shule za Chekechea zinaweza kufikia huduma ya utafsiri bila malipo ili kukusaidia katika lugha yako.

Unaweza pia kuwasiliana nasi au halmashauri ya eneo lako kwa usaidizi. Ili kupata usaidizi katika lugha yako unaweza kupiga Huduma ya Kitaifa ya Utafsiri na Ukalimani kwa nambari 131 450, omba mkalimani apige nambari ya halmashauri ya eneo lako au sisi, na mkalimani atasalia kwenye simu na kutafsiri.

Wakati wa kuomba:

Watoto wanastahiki ESK iwapo watafikisha miaka mitatu kabla ya tarehe 30 Aprili mwaka ambapo wamejiandikisha kuhudhuria shule ya chekechea.

Iwapo siku ya kuzaliwa ya mtoto wako itakuwa kati ya tarehe 1 Januari na 30 Aprili, utahitaji kuhesabu mwaka ambapo wataanza shule ili kufahamu mwaka gani atapata ESK. Unaweza kuchagua kama mtoto wako atahudhuria shule mwaka anapofikisha miaka mitano au sita. Kisha, wanaweza kufikia ESK katika mwaka watakapofikisha miaka mitatu au minne. Iwapo unahitaji usaidizi kuhusu wakati mtoto wako anastahiki ESK, unaweza kuwasiliana na Idara ya Elimu, halmashauri ya eneo lako, muuguzi wako wa afya ya uzazi na mtoto, au chekechea katika eneo lako, au mojawapo ya mashirika yafuatayo katika eneo lako.

  • Laini ya kuuliza maswala ya Chekechea kwa Miaka Mitatu 1800 338 663
  • Brotherhood of St Laurence 03 9483 1183
  • Foundation House 03 9389 8900
  • Huduma za Watoto za Fka 03 9428 4471
  • Kituo cha Maswala ya Wahamiaji Eneo la Kaskazini-Magharibi(Migrant Resource Centre Northwest Region)
    • St Albans: 1300 676 044 or 03 9367 6044
    • Broadmeadows: 03 9351 1278
  • Kituo cha Maswala ya Wahamiaji cha Spectrum 1300 735 653
  • VICSEG New Futures 03 9383 2533
  • Kituo cha Maswala ya Wahamiaji Eneo la Kaskazini-Magharibi(Migrant Resource Centre Northwest Region)
    • St Albans: 1300 676 044 or 03 9367 6044
    • Broadmeadows: 03 9351 1278
  • Kituo cha Maswala ya Wahamiaji cha Spectrum 1300 735 653
  • VICSEG New Futures 03 9383 2533

Reviewed 21 December 2022

Was this page helpful?