Victoria government logo

Kuhusu Zana yako ya Nyenzo za Shule ya Chekechea

Kwa watoto, kucheza na kujifunza huenda pamoja. Kucheza ndivyo jinsi watoto wanavyojitambua na kujielewa na kuelewa ulimwengu wao. Wazazi na familia ni sehemu kuu ya safari hiyo. Kila kitu katika Zana yako ya Nyenzo za Shule ya Chekechea za mtoto wako kimeundwa ili kushirikiwa na kufurahiwa kama familia.

Katika shule ya chekechea, Mfumo wa Masomo na Ukuaji wa Watoto wa Victoria (VEYLDF, Victorian Early Years Learning and Development Framework) hutumiwa kubuni hali za masomo zinazomsaidia mtoto wako kukua na kustawi katika sehemu tano za masomo na ukuaji. Sehemu hizi tano matokeo ni:

  • Utambulisho
  • Jamii
  • Ustawi
  • Masomo
  • Mawasiliano

Michemraba ya kusimulia hadithi

Kusimulia hadithi ni sehemu muhimu ya jinsi watoto wanavyoelewa hali zao za kila siku. Inasaidia kukuza hali ya kujua kusoma na kuandika na inawasaidia kuelewa jinsi ya kuwasiliana na watu walio karibu nao.

Unaweza kumsaidia mtoto wako kujifunza maneno mapya kwa kutumia michemraba hii kwa Kiingereza au lugha nyingine.

  • Weka zamu, taja majina ya picha
  • Jenga pamoja nao
  • Simulia hadithi
  • Uliza maswali

Penseli ya Rangi na Pedi ya Kuchora

Kuchora kwa kutumia penseli ya rangi hutoa njia nyingi za kujifunza:

  • kuboresha ujuzi wa matumizi macho, vidole na mikono kama vile kushika penseli
  • uhusiano wa utendakazi macho na mikono
  • kujifunza kuhusu rangi na maumbo
  • kuonyesha ubunifu na karatasi na nyenzo zingine.

Muhimu zaidi, mtoto wako atajifunza kujieleza kwa usalama na kwa kujiamini. Watoto wengine wanaweza kuwa wanachora alama ambazo huzifahamu na hiyo ni sawa. Huu ni utaratibu wa kawaida wa kujifunza kuchora.

  • Tumia Pedi ya Kuchora ili kuibua mawazo
  • Himiza hali za kuchora kama familia
  • Zungumza unapochora
  • Taja rangi na maumbo

Mbegu

Kupanda mbegu na watoto ni hali ya kujifunza yenye ushahidi mwingi wa kisayansi inayowaruhusu kuona maajabu ya ulimwengu wa asili. Watajifunza juu ya mazingira asili, kukuza lugha na kujifunza kufuata maelekezo rahisi. Watajifunza pia jinsi ya kuchunguza mambo baada ya muda.

  • Zungumza kuhusu mimea na utaje majina ya sehemu zake
  • Ipande pamoja nao
  • Angalia jinsi inavyokuwa kila asubuhi
  • Taja majina ya matunda na mboga sokoni

Kushona Wanyama

Miaka ya utotoni ni wakati ambapo watoto huanza kudhibiti zaidi misuli midogo ya mikono, vidole, vifundo vya mikono, miguu na vidole vya miguu. Kukuza misuli midogo ya mikono na vidole ni muhimu kwa watoto kujitunza na kwa kuandika baadaye. Mtoto wako anaweza kukuza ujuzi wa matumizi ya misuli midogo kwa kutumia udongo wa kuchezea, penseli za rangi au kushona wanyama. Zifuatazo ni baadhi ya njia unazoweza kujifunza kutumia ujuzi wa misuli midogo:

  • Pitisha uzi kwenye mashimo ya mnyama
  • Kufungua na kufunga Zana ya Nyenzo za Shule ya Chekechea
  • Fanya mazoezi ya kufunga zipu au vifungo
  • Kuviringisha udongo wa kuchezea kwa mikono na vidole

Udongo wa kuchezea

Mtoto wako anapotumia udongo wa kuchezea kuunda vitu, anafanya mambo mbalimbali muhimu sana:

  • kuboresha ujuzi wa matumizi ya misuli ya mikono na vidole
  • kutumia hisia zake kutambua vitu
  • kwa kutumia mawazo yake.

Kuunda vitu kwa kutumia udongo wa kuchezea ni sehemu muhimu ya kujifunza kwa mtoto wako.

  • Viringisha udongo uwe kama mpira, ugonge kwa mikono, uponde kwa mikono, ukande
  • Zungumza kuihusu
  • Ongeza vitu vingine kama vile vijiti au manyoya au maganda
  • Tengeneza mitindo kwa kutumia kitu unachoweza kupata

Vitabu vya Watoto

Kusoma vitabu pamoja ni njia nzuri ya kuungana na kukaa pamoja kama familia. Ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za kusaidia kukuza hali ya kujua kusoma na kuandika. Kusimuliana hadithi mara kwa mara na mtoto wako kutaboresha mawazo yake na msamiati.

  • Chagua kitabu pamoja
  • Tafuta mahali pazuri pa kukaa na kusoma
  • Acha wafunguekurasa
  • Tumia sauti tofautikwa wahusika, zungumza kuhusu picha

Watengenezaji wa Muziki

Muziki una manufaa mengi kwa ajili ya kujifunza na ukuaji wa watoto. Kuunda muziki ni njia ya kufurahisha kwa mtoto wako kujifunza maneno mapya, kuimba nyimbo pamoja na familia na kuhisi vizuri kujihusu. Kucheza densi, kuimba, kusonga, kuruka na kucheza kayamba yote ni sehemu ya burudani.

Yafuatayo ni baadhi ya mawazo ya kufurahia muziki na mtoto wako:

  • Cheza densi na kujitikisa kwa wimbo uupendao
  • Hesabu mapigo ili kufunza nambari
  • Jifunze nyimbo fupi zenye vina
  • Tumia kayamba ili kuhesabu silabi kwa maneno

Kasha la Shughuli za Zana

Kasha la shughuli za Zana ni zaidi ya kasha la kubeba vitabu na vitu vya kuchezea - linaweza kutumika kusaidia katika kujifunza na kukua kwa njia nyingi. Mbao nyeupe ni nzuri kwa mchezo wa sumaku, udongo wa kuchezea na kuchora. Kunja Zana iwe kiegemezi. Lalisha Zana chini ili sehemu ya kijani iweze kutumika kwa mchezo wa kubuniwa. Inaweza kuwa eneo la bahari au barabara ya jiji. Onyesha njia unayotumia katika Shule ya Chekechea. Zifuatazo ni baadhi ya zingine za kutumia kasha la Zana:

  • Chora ulimwengu mpya
  • Udongo wa kuchezeazulia la kuchezea
  • Beba kasha lavitabu au vitu vya kuchezea
  • Kama mchezo wa kuigiza

Kasha la shughuli za Zana limeundwa kuwa bidhaa inayofaa kwa mazingira. Limetengenezwa kwa nyenzo zinazoweza kutumika tena, panapowezekana na limeundwa ili kutumiwa tena kama kumbukumbu ya kuhifadhi kumbukumbu za shule ya chekechea za mtoto wako.

Kujenga Jamii

Victoria ni jamii yenye watu mbalimbali, nyumbani kwa tamaduni nyingi na lugha tofauti zinazozungumzwa. Utofauti ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Vitu vilivyo kwenye Zana vinaendeleza mazungumzo kuhusu jamii mbalimbali.

  • Kwa watoto, kucheza na kujifunza huenda pamoja. Kucheza ndivyo jinsi watoto wanavyojitambua na kujielewa.
  • Tumia udongo wa kuchezea ili kujifanya unatengeneza chakula cha tamaduni zingine au utamaduni wako.
  • Cheza kayamba ukiwa unasikiliza muziki wa jadi kutoka kwenye tamaduni zingine au utamaduni wako
  • Zungumza na mtoto wako kuhusu nchi nyingine na wanyama wake wa asili

Vitabu vya Kiauslani

Vitabu vyote vilivyojumuishwa kwenye Zana ya Nyenzo za Shule ya Chekechea ya 2023 vina tafsiri za Kiauslani. Kiauslani na manukuu yamejumuishwa kwenye video pia.

Kiauslani ni lugha ya ishara inayotumiwa na idadi kubwa ya jamii ya Viziwi ya Australia na pia ni sehemu ya Mpango wa Lugha za Watoto wa Victoria unaopatikana katika baadhi ya Shule za Chekechea za Watoto wa Umri wa Miaka Minne.

Wataalamu wa elimu wametambua kuwa kuna manufaa mengi kwa watoto kujifunza kwa lugha nyingine wakiwa na umri mdogo, ikijumuisha:

  • kukuza ujuzi wa kabla ya kusoma na kabla ya kuandika
  • wepesi wa kutambua mambo
  • kukuza hali ya kujiamini na ustawi
  • kuimarisha hali ya kujitambua.

Kuheshimu Utambulisho

Tamaduni zawatu wetu Wenyeji ni sehemu muhimu ya historia ya Australia. Kuhimiza watoto wote kujifunza kuhusu tamaduni zote hujenga ufahamu, kukubali na fahari. Tunajivunia kusherehekea waandishi na watengenezaji wetu Wenyeji katika Zana. Miundo ya hadithi, kwa mfano, inaonyesha utamaduni thabiti wa kusimulia hadithi wa Wenyeji. Zifuatazo ni baadhi ya shughuli zinazomsaidia mtoto wako kujifunza zaidi kuhusu mila na tamaduni za Wenyeji:

  • Jifunze kuhusu alama za wanyama au vitu za Wenyeji
  • Zungumza kuhusu viongozi wa asili au mashujaa wa michezo
  • Pata maelezo zaidi kuhusu tamaduni na watu wa Asili

Ustawi na Msaada wa Ziada

Watoto wote hujifunza kwa njia tofauti na kwa utaratibu wao wenyewe. Zana ya Nyenzo za Shule ya Chekechea inampa mtoto wako vitabu na vitu vya kuchezea ambavyo vinaweza kutumika kwa njia nyingi tofauti ili kushughulikia uwezo wote. Lakini wakati mwingine unahitaji msaada wa ziada kwa masomo ya mtoto wako. Ikiwa unafikiri kuwa wewe au mtoto wako atahitaji msaada wa ziada, kuna njia kadhaa unaweza kufanya hivyo:

  • Walimu wa shule ya chekechea wa Victoria wana ujuzi na maarifa ya kusaidia. Zungumza na mwalimu wa mtoto wako kuhusu masuala ya mtoto wako
  • Weka miadi ya kuonana na daktari wako au muuguzi wa afya ya uzazi na watoto ili kuzungumzia masuala yako
  • Wasiliana na Parentline kwa nambari 13 2289 kwa ushauri na msaada wa faragha

Reviewed 21 February 2023

Was this page helpful?