Victoria government logo

Chekechea ya Kuanza Mapema (Early Start Kindergarten) - Kiswahili (Swahili)

Ikiwa unatokea kwenye asili ya ukimbizi au mtafuta hifadhi unaweza kustahiki Chekechea ya Kuanza Mapema (ESK). ESK inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa unapata kiwango cha juu zaidi cha saa za mpango wa chekechea ya watoto bila malipo kila wiki kwa ajili ya mtoto wako.

Mnamo 2023, programu za Chekechea ya Mtoto wa Miaka Mitatu ni za kati ya saa 5 na 15 kila wiki na programu za Chekechea ya Watoto wa Miaka minne ni za saa 15. Kujiandikisha kupitia ESK kunahakikisha saa 15 kamili kila wiki katika programu za Chekechea ya Watoto wa Miaka Mitatu na Miaka minne. Inapatikana kwa watoto ambao:

  • wanatoka katika mazingira ya mkimbizi au mtafuta hifadhi
  • wanaojitambua kama Waaboriginal na/au Torres Strait Islander
  • ambaye familia yake imewahi kuwa na mwingiliano na ulinzi wa mtoto(child protection)

Haijalishi ni wapi wanaishi Victoria watoto hawa wanaweza kupata saa 15 bila malipo za chekechea kwa wiki wakati wa kipindi cha kuanzisha hii programu. Ufikiaji wao wa sasa na saa wanazopokea hazitabadilika.

Jinsi ya kuomba:

ESK inapatikana katika programu zote za chekechea zinazotolewa na mwalimu aliyehitimu. Unaweza kumwandikisha mtoto wako kwa kuwasiliana na chekechea iliyo karibu nawe na kuomba kupata ruzuku ya Chekechea ya Kuanza Mapema. Huduma za Chekechea zinaweza kufikia huduma ya utafsiri bila malipo ili kukusaidia katika lugha yako.

Unaweza pia kuwasiliana na Idara ya Elimu ya Shule ya Chekechea ya Miaka Mitatu kupitia Simu ya Maulizo kwa 1800 338 663 au baraza lako la mtaa kwa usaidizi. Ili kupata usaidizi katika lugha yako unaweza kupiga simu kwa Huduma ya Kitaifa ya Utafsiri na Ukalimani kwa nambari 131 450, omba mkalimani apige simu nambari ya halmashauri ya eneo lako au Idara ya Elimu, na mkalimani atakaa kwenye simu na kutafsiri.

Wakati wa kuomba:

Watoto wanastahiki ESK iwapo watafikisha umri wa miaka mitatu kabla ya tarehe 30 Aprili mwaka ambapo wamejiandikisha kuhudhuria shule ya chekechea. Tazama ‘ni lini kujiandikisha’.

Unaweza kuchagua kama mtoto wako atahudhuria shule katika mwaka anapofikisha miaka mitano au sita. Kisha, wanaweza kufikia ESK katika mwaka watakapofikisha umri wa miaka mitatu au minne.

Iwapo unahitaji usaidizi kuhusu wakati mtoto wako anastahiki ESK, unaweza kuwasiliana na Idara ya Elimu, halmashauri ya eneo lako, muuguzi wako wa afya ya uzazi na mtoto, au chekechea katika eneo lako, au mojawapo ya mashirika yafuatayo katika eneo lako.

  • Laini ya kuuliza maswala ya Chekechea kwa Miaka Mitatu 1800 338 663
  • Brotherhood of St Laurence 03 9483 1183
  • Foundation House 03 9389 8900
  • Huduma za Watoto za Fka 03 9428 4471
  • VICSEG New Futures 03 9383 2533

Reviewed 25 September 2023

Was this page helpful?